LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaingia Raundi ya 19 kesho
(Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar
es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.
Yanga itakuwa
mgeni wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika mechi itakayofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nayo Kagera Sugar inaikaribisha Rhino
Rangers ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba.
Uwanja wa Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro ndiyo
utakaotumika kwa mechi kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati
Coastal Union itaumana na Mbeya City katika mechi itakayooneshwa moja
kwa moja na Azam Tv kutoka Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Maafande wa
Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Mgambo Shooting katika mchezo
utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid
jijini Arusha.
Jumapili (Februari 23 mwaka huu) katika Uwanja
wa Taifa ni Simba dhidi ya JKT Ruvu, mechi ambayo pia itaoneshwa moja
kwa moja na Azam Tv.
Mechi kati ya Azam na Tanzania Prisons
iliyokuwa ichezwe kesho (Februari 22 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi sasa
itachezwa Jumapili (Februari 23 mwaka huu) ambapo na itakuwa ‘live’.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya
Ashanti United na Azam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex
(Chamazi).
Wakati huo huo: Michuano ya mikoa katika mpango
maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuboresha Taifa
Stars inaanza kutimua vumbi kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi nne.
Mechi
rasmi ya ufunguzi wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager itakuwa kati ya Ilala na Temeke. Mechi hiyo ya kundi G
itachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia saa 9.30 alasiri.
Kundi
A kutakuwa na mechi kati ya Pwani na Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini
mjini Mlandizi wakati Kusini Unguja na Kaskazini Unguja zitacheza
kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja katika kundi H.
Kusini Pemba na Kaskazini Pemba zitacheza mechi ya Kundi I katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Mechi
za keshokutwa (Februari 23 mwaka huu) ni Simiyu itacheza na Shinyanga
mjini Bariadi katika kundi E. Nayo Ruvuma itacheza na Njombe kwenye
Uwanja wa Majimaji mjini Songea katika kundi D.
Kundi C ni
Tanga na Kilimanjaro kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati Kagera itacheza
na Geita kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika kundi B. Mtwara
itacheza na Lindi kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara katika kundi
F.
Wang’amuzi 40 wa vipaji tayari wamesharipoti kwenye vituo vya mechi hizo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment